Rasmi Fabrice Luamba Ngoma ni Nyota wa Simba SC baada ya kusaini Kandarasi ya Miaka Miwili na Wekundu wa Msimbazi Simba SC. Tumezungumza na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally kuhusu Usajili huo kuanzia Mchakato wa kumapata na Kandarasi husika. Kuhusu Nyota wapya kuingia Kambini Nchini Uturuki Ahmed ametaja Tarehe husika ya Nyota hao kuanza Safari. Maswali kuhusu kuangwa kwa Jonas Mkude Siku ya Simba Day pia yamejibiwa hapa na Ahmed Ally. Kuhusu Chama Ahmed amewatoa hofu wana Simba pasina kusahau Kijembe kwa Watani zake kuhusu Fiston Mayele kuondoka Yanga.