Yanga SC imetangaza rasmi kuwa imemsajili Augustine Okrah raia wa Ghana kutoka Klabu ya Bechem ya kwao Ghana, Okrah ametambulisha muda huu katika uwanja wa Amaan Zanzibar na amewahi kuichezea Simba SC.
Kocha Manqoba Mngiqithi (55) Raia wa AFRIKA Kusini ametangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC akitokea Klabu ya Gorden Arrows ya Afrika Kusini. Mngiqithi ana uzoefu mkubwa wa mashindano ya CAF na Ligi za kiafrika kutokana kufanya kazi na Klabu ya Mamelod Sundowns kwa muda mrefu toka 2013 Hadi 2024 akiwa anashika nafasi mbalimbali.