Clatus Chama amerudi Leo July 4 kutoka kwao Zambia kwenye mapumziko baada ya kumaliza Msimu na sasa amerejea kujiandaa na Msimu 2023/2024. Clatus amewapongeza Wachezaji walioanzisha Michezo ya Bonanza kwa lengo la kuridisha kwa jamii, amekiri kuwa anatamani kufanya kama wanavyofanya wao. Aidha Clatus ameeleza namna alivyopokea taarifa ya kuagwa kwa Jonas Mkude na Erasto Nyoni kwani ni Wachezaji aliwazoea sana na wamekuwa na kiwango bora sana. Baada ya kuwa na Msimu mgumu wa kutokuwa na Mataji Chama amewaomba Mashabiki kuwaamini na ameahidi kupambana na Msimu huu kuwa kutafuta mataji. Sanjari na hayo Clatus amepongeza Wachezaji waliofanya vizuri Msimu uliopita na ameahidi kufanya vizuri Msimu ujao na kurudi kwenye kinyang'anyiro cha MVP.
JE, UNA JAMBO LAKO? USILIFICHE! 🌍 Kuwa wa kwanza kutujuza habari, matukio, au matangazo kupitia MPENJA TV. Sisi tupo hapa kwa ajili yako! 🔴 TUPIGIE/WHATSAPP: +255 748 101 101 📞 SIMU: +255 686 816 895 | +255 686 715 249 📧 EMAIL: mpenjatvtz@gmail.com