EXCLUSIVE: MAYELE KUBAKI AU KUONDOKA YANGA?/MWENYEWE AWEKA WAZI/"MIMI NDIO NAAMUA NICHEZE WAPI” by @Mpenja TV - Post Details

EXCLUSIVE: MAYELE KUBAKI AU KUONDOKA YANGA?/MWENYEWE AWEKA WAZI/"MIMI NDIO NAAMUA NICHEZE WAPI”

Karibu kutazama Exclusive interview na Fiston Mayele, Nyota wa Kimataifa wa Congo na MVP wa Ligi Kuu ya NBC Msimu 2022/2023. Mayele ameweka sawa tetesi za kuondoka Yanga na amewatoa hofu Mashabiki wa Yanga kuwa maongezi bado yanaendelea hivyo lolote linawezekana. Aidha Fiston ameshukuru Mashabiki wa Yanga kwa Upendo wanaonyesha kwake pamoja na utofauti wa Mashabiki wa Congo na Tanzania na amekiri kuwa Mashabiki wa Tanzania wanapenda Mpira kuliko Congo. Amejibu maoni ya Wadau kuhusu kuwa Mchoyo Uwanjani haswa kwenye nafasi za kufunga na ameeleza kiupana sana kwanini huwa anafanya hivyo na hana pasi nyingi za Mwisho. Sanjari na hayo Mayele ameeleza ukaribu wake na Wachezaji ambao wamepewa Mkono wa kwaheri na Yanga na namna alivyopokea taarifa hizo. Mwisho kabisa Fiston ametaja Kikosi chake bora Msimu uliokwisha.

Similar Posts!