Ally Kamwe ametoa sifa za kutosha kwa Kiungo Jonas Mkude 'Nungu nungu' kuwa ni kiungo bora wa mkabaji kwa hapa Tanzania. Aidha Kamwe ameeleza kuwa Jonas anaweza kucheza Timu yoyote Tanzania hata Young Africans kuna uwezekano wa Jonas kucheza. Sanjari na hayo Ally amejibu maswali ya Chemsha bongo na kuimba Wimbo ambao anausilikiliza sana kipindi hiki ambacho Ligi imekwisha.