Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ally Kamwe ametua Dodoma na kulakiwa na Mashabiki wa Yanga. Safari ya kuelekea Rwanda kituo cha kwanza kupumzika baada ya kuanzia Dar Es Salaam ni Dodoma ambapo Semaji la Wananchi amepata Nyama Choma pamoja na Mashabiki wa Yanga. Pia ameeleza namna Safari ilivyo mpaka sasa na kituo kinachofuata kwa mapumziko ni Kahama kisha kuitafuta Kigali Rwanda.
Leo Mei 13,2024 Mtibwa Sugar inashuka Dimba la Manungu Turiani kumenyana na Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC,,Saa 10 jioni.