KOCHA WA ZAMANI MAMELOD APEWA MKATABA YANGA SC by @Millard Ayo - Post Details

KOCHA WA ZAMANI MAMELOD APEWA MKATABA YANGA SC

Kocha Manqoba Mngiqithi (55) Raia wa AFRIKA Kusini ametangazwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC akitokea Klabu ya Gorden Arrows ya Afrika Kusini. Mngiqithi ana uzoefu mkubwa wa mashindano ya CAF na Ligi za kiafrika kutokana kufanya kazi na Klabu ya Mamelod Sundowns kwa muda mrefu toka 2013 Hadi 2024 akiwa anashika nafasi mbalimbali.

Similar Posts!

ALLY KAMWE ALIVUJISHA HII YA MWALIMU ILA HATUKUMZINGATIA KABISA
ALLY KAMWE ALIVUJISHA HII YA MWALIMU ILA HATUKUMZINGATIA KABISA

Yanga SC imewashangaza mashabiki wa soka Leo baada ya kutangaza kukamilisha usajili wa aliyekuwa Mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya Morocco Selemani Mwalimu. Mwalimu msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Simba SC akitokea Wydad, hata msimu huu 2026/27 Jumamosi ya Agosti 8 2026 kwenye Simba Day alitambulishwa tena kuwa atakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu mwingine wa mkopo. Haileweki nini kimetokea na kama Yanga SC wamemsajili Moja kwa Moja au kwa mkopo ila Agosti 4 Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe alitamba kuwa "Wanafanya nae mazoezi lakini mchezaji wetu" wakati huo Mwalimu alikuwa Kigali Rwanda na Simba SC wakijiandaa na msimu mpya.



LIVE: SIMBA DAY, NYOMI LA WANASIMBA UWANJA WA UHURU
LIVE: SIMBA DAY, NYOMI LA WANASIMBA UWANJA WA UHURU

Tazama MBASHARA shamrashamra za madhimisho ya miaka 90 SIMBA DAY



LIVE: SHALULILE ATUA JANGWANI, ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
LIVE: SHALULILE ATUA JANGWANI, ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

PETER SHALULILE KWA MARA YA KWANZA AMEWASILI KWENYE OFISI ZA MAKAO MAKUU YA YANGA JANGWANI



YANGA SC WATAMBULISHA WHAT A PLAYER 6
YANGA SC WATAMBULISHA WHAT A PLAYER 6

Yanga SC imemtanbulisha Kiungo wake mpya namba 6 Fred Ngoma (28) Raia wa Congo Brazzaville, Ngoma anajiunga na Yanga SC akitokea Olympique de Safi ya Morocco.