Mshambuliaji wa kimataifa wa Serbia anayeichezea Simba SC Dejan Georgijevic (28) leo ametangaza kuwa amevunja mkataba wake wa Simba SC, Dejan ameeleza hayo ikiwa ni siku 53 zimepita toka ajiunga na Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu na kumfanya kuwa mchezaji mwenye mkataba mrefu zaidi Simba SC.