Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wamevunja mwiko wa kutokushinda mbele ya Lipuli FC baada ya leo kuichapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa. Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili dakika ya 5 na 44 huku bao la tatu likifungwa na Meddie Kagere dakika ya 57 wakati bao pekee la Lipuli likifungwa na Paul Nonga dakika ya 18. Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 48 kwenye nafasi ya tatu ikiwa ni pointi 2 nyuma ya Azam wanakamata nafasi ya pili, huku Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 61.