Baada ya aliekuwa Staa wa Simba SC raia wa Zambia Cloutous Chama kujiunga na club ya RS Berkane ya nchini Morocco. Sasa aliekuwa Msemaji wa Simba Sc, Haji Manara ameyaandika haya . . "Niliona miguu yako siku ya kwanza nikapagawa na ufundi wako..Nakumbuka tukiwa Kitwe Zambia,Picha hiyo ya mbele ikatawala Katika mitandao na Magazeti ya kwenu"- Haji Manara . . "Nakumbuka pia wakati tunarudi ukaniambia tutafuzu kwenye mechi ya marudiano, ahhhhh Mwamba ukafunga goli maridadi mno dhidi ya Nkana"- Haji Manara "Real friend na Jirani yangu nikutakie kheri nyingi katika maisha mapya Morocco na naamini utafanikiwa"- Haji Manara
Yanga SC imewashangaza mashabiki wa soka Leo baada ya kutangaza kukamilisha usajili wa aliyekuwa Mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya Morocco Selemani Mwalimu. Mwalimu msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Simba SC akitokea Wydad, hata msimu huu 2026/27 Jumamosi ya Agosti 8 2026 kwenye Simba Day alitambulishwa tena kuwa atakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu mwingine wa mkopo. Haileweki nini kimetokea na kama Yanga SC wamemsajili Moja kwa Moja au kwa mkopo ila Agosti 4 Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe alitamba kuwa "Wanafanya nae mazoezi lakini mchezaji wetu" wakati huo Mwalimu alikuwa Kigali Rwanda na Simba SC wakijiandaa na msimu mpya.
Tazama MBASHARA shamrashamra za madhimisho ya miaka 90 SIMBA DAY
PETER SHALULILE KWA MARA YA KWANZA AMEWASILI KWENYE OFISI ZA MAKAO MAKUU YA YANGA JANGWANI
Yanga SC imemtanbulisha Kiungo wake mpya namba 6 Fred Ngoma (28) Raia wa Congo Brazzaville, Ngoma anajiunga na Yanga SC akitokea Olympique de Safi ya Morocco.