Vijana wengi kwa sasa wanamtazama Mbwana Samatta kama kioo chao katika mchezo wa soka ukizingatia amefika level za juu katika soka hakuna mtanzania aliyefikia level yake, Amplifaya ya Clouds FM Leo imepiga nae stori na kutaka kujua mambo mbalimbali katika soka.
Yanga SC imewashangaza mashabiki wa soka Leo baada ya kutangaza kukamilisha usajili wa aliyekuwa Mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya Morocco Selemani Mwalimu. Mwalimu msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Simba SC akitokea Wydad, hata msimu huu 2026/27 Jumamosi ya Agosti 8 2026 kwenye Simba Day alitambulishwa tena kuwa atakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu mwingine wa mkopo. Haileweki nini kimetokea na kama Yanga SC wamemsajili Moja kwa Moja au kwa mkopo ila Agosti 4 Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe alitamba kuwa "Wanafanya nae mazoezi lakini mchezaji wetu" wakati huo Mwalimu alikuwa Kigali Rwanda na Simba SC wakijiandaa na msimu mpya.
Tazama MBASHARA shamrashamra za madhimisho ya miaka 90 SIMBA DAY
PETER SHALULILE KWA MARA YA KWANZA AMEWASILI KWENYE OFISI ZA MAKAO MAKUU YA YANGA JANGWANI
Yanga SC imemtanbulisha Kiungo wake mpya namba 6 Fred Ngoma (28) Raia wa Congo Brazzaville, Ngoma anajiunga na Yanga SC akitokea Olympique de Safi ya Morocco.