Mchezaji wa Simba SC Kibu Dennis ambaye hivi karibuni Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen alimuacha kikosini kwa madai ya kushughulikiwa kwa suala la utata wa uraia wake, leo amerejeshwa kikosini ikiwa ni siku chache zimepita toka mamlaka zitangaze kuwa amepatiwa uraia, Kibu leo amejumuika na wachezaji wenzake wa Taifa Stars wanaojiandaa na michezo miwili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar dhidi ya Benin #