Dream Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!

“”

 Report User

Highlights

SIMBA KUPEWA POINT 3 ZA MEZANI BAADA YA EL MERREIKH KUCHEZESHA WACHEZAJI WENYE ADHABU,C.E.O AFUNGUKA
SIMBA KUPEWA POINT 3 ZA MEZANI BAADA YA EL MERREIKH KUCHEZESHA WACHEZAJI WENYE ADHABU,C.E.O AFUNGUKA

Nimepata taarifa za El Merreikh kujumusha wachezaji 3 kwenye mechi vs Simba ingawa walifungiwa miezi 6 baada kusaini kandarasi na vilabu 2 tofauti (El Hilal na El Merreikh) wachezaji hao ni Mohamed AlRashed Mahamoud, Ramadan Agab, Baljit Khamis Mohamed Kwa mujibu wa kanuni ya CAF ya VI(10) timu itakayochezesha mchezaji asiye halali itapoteza mchezo na kuondolewa mashindanoni 👉 Kwa mujibu wa barua ambayo El Merreikh waliyopewa ni wazi kuwa walichezesha wachezaji ambao hawakustahili Hivyo Simba wana haki ya kwenda kushtaki CAF SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa. Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonyesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA) Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionyesha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili "Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita. Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez. Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni "Timu itakayomchezesha mchezaji aliyesimamishwa au asiyeruhusiwa itahesabika imepoteza mchezo husika na moja kwa moja itaondolewa mashindanoni ikiwa kamati ya mashindano ya Caf itajiridhisha na hoja zitakazowasilishwa," inasema kanuni ya saba.



LWANGA NA WAWA HAWATACHEZA  MECHI IJAYO KIMATAIFA DHIDI YA EL MERREIKH KWA MKAPA,SABABU HII
LWANGA NA WAWA HAWATACHEZA MECHI IJAYO KIMATAIFA DHIDI YA EL MERREIKH KWA MKAPA,SABABU HII

Wachezaji @SimbaSCTanzania Thaddeo Lwanga na Pascal Wawa watakosa mechi ya ijayo dhidi ya @ElMerreikhSDN Dsm wana Yellow Card 2 kila mmoja walizopata(As Vita na El Merreikh). Pia Wachezaji 2 wana Yellow card 1 kila mmoja ni Shomari Kapombe(Simba) na Tajeldin Elnour(El Merreikh.) Sometimes.. Football ni mchezo wa hesabu. Ukizielewa, utaelewa walichokifanya Simba 🦁 Leo mbele ya Al Merrikh Uongozi wa Simba uliwekeza kiwanjani kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu na ubora Wakawekeza tena kwenye benchi la Ufundi kwa kuajiri wataalam wenye uzoefu/ubora wa kusoma mbinu za mpinzani na kupata majibu yake Kuna kocha Mkuu Didier Gomes. Kuna Seleman Matola.. Halafu kuna yule Performance analyst kutoka Zimbabwe, Calvin Mavhunga Jopo la watu hawa, ukiongeza na wataalamu wa viungo, ni ishara kuwa Simba ilijiandaa kuwa washindani wa kweli AFRIKA Sina maana kwamba hawatafungwa. Even Barcelona ile ya Pep Guardiola iliwahi kupoteza mechi.. Ninachokimanaisha hapa, Uongozi wa Simba umefanya kazi kubwa ya kuijenga Timu yao msimu huu Robo fainali waliyocheza msimu wa 2018/19 ilikuwa ya 'fluke' tu, ila hii watakayocheza msimu huu (Asilimia 70 wameshafika), Wamejiandaa nayo Haya yanayotokea sasa, hayatokei kwa bahati mbaya. Kuna HATUA UONGOZI WA SIMBA WALIZICHUKUA👍 Hongera kwao @simbasctanzania @moodewji @bvrbvra @crescentius_magori 👏



UONGOZI WA SIMBA WAJA NA KAULI HII BAADA YA USHINDI MBELE YA JKT TANZANIA
UONGOZI WA SIMBA WAJA NA KAULI HII BAADA YA USHINDI MBELE YA JKT TANZANIA

UONGOZI WA SIMBA WAJA NA KAULI HII BAADA YA USHINDI MBELE YA JKT TANZANIA



UJUMBE MZITO KUTOKA  KWA ONYANGO NA MIQUISSONE WATUMWA KUTOKA AL AHLY
UJUMBE MZITO KUTOKA KWA ONYANGO NA MIQUISSONE WATUMWA KUTOKA AL AHLY

BAADA ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba, Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane, ameibuka na kutamka kuwa Simba ilikuwa kwenye ubora zaidi ya wao.Kocha huyo alisema kati ya nyota ambao aliwaona ni hatari kwao ni mfungaji pekee wa bao hilo, Luis Miquissone na beki wa kati, Joash Onyango. Akizungumza na Spoti Xtra, kocha huyo raia wa Afrika Kusini, alisema katika mchezo huo wachezaji wake hawakuwa na kasi anayoifahamu tofauti na wapinzani wao Simba walioonekana kulishambulia goli lao dakika zote tisini. Kocha huyo alisema Simba walitumia vema udhaifu wao na kufanikiwa kupata ushindi huo “Niwe muwazi tu kwa kusema hatukuwa na kasi uwanjani na Simba wakawa bora, hivyo wakatumia vema udhaifu wetu kutudhuru na kufanikiwa kupata pointi tatu dhidi yetu. “Simba walifanikiwa kucheza kwa nguvu na kujilinda vizuri kwa dakika zote 90. Walikuwa makini katika kuokoa mipira yote ya hatari iliyokuwa inafika golini kwao. Wachezaji hatari alikuwa mwenye namba 11 (Luis) na 16 (Onyango),” alisema Mosimane.



SIMBA YAZUA BALAA Misri Hapakaliki, KOCHA Wa AL AHLY Pitso Kufukuzwa Baada ya Kufungwa na SIMBA
SIMBA YAZUA BALAA Misri Hapakaliki, KOCHA Wa AL AHLY Pitso Kufukuzwa Baada ya Kufungwa na SIMBA

SIMBA YAZUA BALAA Misri Hapakaliki, KOCHA Wa AL AHLY Pitso Kufukuzwa Baada ya Kufungwa na SIMBA #CAFCL​



MANARA AOMBA RADHI KWA SIMBA KUSHINDA USHINDI MWEMBAMBA VS AL AHLY|"SIMBA NDIO KAIMU BINGWA AFRIKA"
MANARA AOMBA RADHI KWA SIMBA KUSHINDA USHINDI MWEMBAMBA VS AL AHLY|"SIMBA NDIO KAIMU BINGWA AFRIKA"

MANARA AOMBA RADHI KWA SIMBA SC KUSHINDA USHINDI MWEMBAMBA VS AL AHLY|"SIMBA NDIO KAIMU BINGWA AFRIKA"




« Previous Next »


User Detail Page

You can find user latest posts and related content on the page. Friends, comments for events / matches are also available on the page. Even you can find users who are same pleasure with current user.

#Travel, #SupportYourTeam, #AllAboutSports