Dream Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Mambo 10 nilioyaona Simba vs Dodoma 1: WHAT A MATCH. Tactically, Technically makocha na wachezaji wametupa dakika 90 zilizoshiba. Mechi ya nguvu, kasi na maarifa ya kutosha.. 2: Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata aliingia na 4-2-4 akiwa na viungo wawili tu katikati ya kiwanja. Watu wanne wa juu wakiwa bora sana kwenye pressing 🙌 Game Plan ilikuwa sahihi, 'Quality' ikatofautisha ubao wa matokeo. Nafasi ambazo Dodoma walizichezea, Simba walizitumia. 3: Dakika 45 za kwanza, Didier Gomes alibaki na sytem ya 4-2-3- 1 lakini akabadili style of Play kidogo. Chama akaenda pembeni, Bwalya akacheza zone ya 14. Timu ikaonekana nzito kidogo 'kulink' kutoka kati kuingia phase ya 3 ya kiwanja. Nini alifanya? 4: Akamtoa Muzamir Yassin akamuingiza Morrison. Chama akarudi kwenye zone ya 14, Bwalya akarudi kati. Timu ikalainika, nafasi zinakapatina. 5: Again, Simba wamethibitisha tena nilichowahi kukisema. Ni timu hatari pindi inaposhambuliwa. Mpinzani akitawanyika wana watu wazuri wa kutega kwenye maeneo ya wazi. Wakiupata mpira.. hawachezi, wanashambulia. 6: CHAMA 🐐.. Damu ya Zambia. mwili wa Hispania. Akili ya Brazil.. Alichobakisha ni kutoa asali na maziwa kwenye miguu yake.. What A Player 🙌 Anaufanya mchezo wa mpira uonekana mrahisi sana. Yuko Sharp kwenye kujitengenezea nafasi na ni mtulivu kwenye maamuzi yake 7: Ule mguu wa kushoto wa Larry Bwalya una 'vision' ya ajabu sana🙌 Ana utulivu sana. Anaimeza presha ya Opponent kwa ustadi wa aina yake. Ile pivot yake na Nyoni inawapa uhakika Simba wa kumiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo 8: Justine Omary🙌 Yule beki wa kati wa Dodoma Jiji.. Ni mpambanaji sana. Ana kimo kizuri, ana nguvu na timing yake ni nzuri sana. Akisukuma kidogo kwenye kutafuta kasi, he is one of the best tunaoweza kuwategemea kwa baadae 9: Miquissone 👍 Katika ubora wake wa kila siku. Dodoma walimpa mechi ngumu akawafunga bao gumu. Ule ndio ubora unaowabeba Simba wanapokuwa katika nyakati ngumu kiwanjani 10: Mkandala 👍 Alipambana sana kumvuruga Muzamir katikati ya kiwanja. Wale mabeki wa pembeni wa Dodoma, George Wawa na Ngalema wamevuja sana jasho. Well done kwao.. Nb: Tar 8 bebeni Tende tu.. Ftari mtaipata KWA MKAPA 😀
Mambo 10 nilioyaona Gwambina vs Simba 1: MNYAMA 🦁 ON TOP OF THE TABLE🙌 Kibabe. Kikatili Simba wameondoka na Pointi 3 ngumu ndani ya pitch kigumu kule Misungwi. MO aanze kuagiza masweta sasa.. Kileleni baridi 😀 2: Asante kocha wa Gwambina, Mohammed Badru👏 Asante Didier Gomes.. 👍 Licha ya changamoto ya pitch, makocha wametupa mechi nzuri kwenye mbinu. Kasi, nguvu na maarifa yalitawala kwa Dakika 90🙌 3: Gwambina walikuja na system ya 4-2-3-1, Kati wakianza na Holding wawili. Baraka Mtui na Kagoma walikuwa na utulivu na kasi ya kupokonya mpira huku Viungo watatu wa juu, Meshack, Jimmson na Rajab wakiwa wakiwapress vyema mabeki wa Simba ili kuwanyima nafasi ya kuanza shambulizi kwa kupiga 'Long Balls' 4: Didier Gomes aliswitch kutoka kwenye 4-2-3-1 na kuja na 4-1-3-2 akiwa na Plan ya kucheza kwa mipira mirefu, akiutoa mpira katikati ya kiwanja kukwepa changamoto ya pitch 5: Always.. Mechi ngumu kwenye mbinu huamuliwa na 'quality' za wachezaji kuamua mchezo. Hapa ndipo tofauti ilipokuja.. Quality ya Simba ikaidhibu Gwambina. Kivipi? 6: Rudi na ulitazame tena na tena bao la MOHAMMED HUSSEIN🙌 Moderm Football it's all about Space and Time. Ile First touch ya Tshabalala ni ya Thamani sana. Ndani ya sekunde chache mpira ukiwa angani, brain yake ikafikiri kwa haraka na kuamua.. WHAT A GOAL🙌 7: Gwambina imepoteza lakini Yule kipa wao Mohammed Makaka alikuwa kwenye kiwango bora sana 👍 Simba walicheza kwa malengo na Attempt zao zilikuwa ON TARGET.. Mikono ya Makaka ilikuwa kwenye ubora sana. 8: Onyango🙌 INATOSHA SASA KUMUELEZEA. Kile ni KITASA cha Guantanamo 🙌 Anacheza kwenye kila mdundo wa mpinzani. Ukiweka Reggea, mnaruka nae. Ukiweka singeli, mnalimwaga nae.. What A Player🙌 9: Lile tukio la Onyango linabaki kwenye maamuzi ya Line 1. Katika mstari aliosimama, yeye ndio mwenye nafasi ya kuona vyema muelekeo wa ule mpira ukiwa angani 10: Welld done Jimmson Mwanuke💪 Mchezaji mkubwa kwenye jezi ya timu ndogo. Anajua sana. WELL PLAY GUSTAVO. Na udogo wake vilevile, Alimstopisha Kisinda na leo kammeza Morrison.. Nb: Kwani Wananchi wenyewe Wanasemaje 😀
TAZAMA MSEMAJI WA MTIBWA SUGAR T.KIFARU ANYOSHA MIKONO "SIMBA NI HATARI SANA AFRIKA /WANAPIGA PASS MILION 2
Mechi tamu ambayo timu zimeonyesha ubora mpaka filimbi ya mwisho, huwezi kujutia kwanini ulichelewa kulala kama umeshuhudia mechi hii katika dakika zote. Ilikuwa iko wazi kabisa kuwa ni mechi ambayo Ahly alihitaji alama 3 ili kufuta uteja baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo mbele ya Simba. Kuna kitu Gomes amekipandikiza katika fikra za wachezaji wa Simba nako ni kujua kuwa jukumu la kuzuia si la watu fulani wachache ndani ya timu. Wakati ambao Simba haina mpira unaona wachezaji wote wanafanya mikimbio ya haraka kuhakikisha kuwa wanakuwa nyuma ya Mpira. Hiki si kitu ambacho tulikuwa tukikiona huko nyuma, kwanza timu haikuwa na nidhamu hasa wanapoupoteza mpira. Wachezaji wanajigawa mafungu mawili, kuna wale ambao wanazuia na wengine wanaamini kukaba si sehemu ya majukumu yao. Leo Simba ilicheza kwa tahadhari kubwa hasa wakati ambao Ahly wanamiliki mpira, kwanza hawakukubali kuvunja umbo lao na walikubali kuwa wadogo mbele ya mpinzani. Mbele alibaki Meddie Kagere ili kusubiri mashambulizi ya haraka pale ambapo Simba itafanikiwa kuunasa Mpira. Kwa bahati mbaya tu ni kuwa mashambulizi mengi ya Simba yalizuia na Ahly baada ya kuwa compact sana katika eneo lao. Ahly ilishajua kuwa Simba ina wachezaji wawili ambao ni hatari hasa katika eneo la mbele. Kongole kwa Pitso kwa sababu mabadiliko makubwa ya kikosi aliyoyafanya yaliendana na mahitaji ya mchezo wa leo. Ahly ilifanikiwa kuua movement nyingi za Simba kwa kuzuia wachezaji wanaohusika na build up nyingi za Simba. Kwanza ni Luis, wakahakikisha kuwa hawi na madhara kwa kumnyima uhuru wa kufanya mikimbio kutokea pembeni . Wa pili ni Chama, kila aliposhika Mpira kuna wachezaji wawili walimzonga ili kuhakikisha haoni ni wapi aipeleke pasi yake ya kwanza . Kikubwa zaidi wachezaji wa Simba wanajiamini sana wakiwa na mpira, timu nyingi za Tanzania zinapokuwa ugenini huoni wakipiga pasi na kufika katika eneo la mpinzani. Heko kwa Simba, kuna muda waliiweka Ahly katika nyakati ngumu na kama wangeongeza umakini pengine wangeondoka na sare kama sio kushinda mechi kabisa. Ni nafasi moja pekee ambayo imeamua matokeo, mbali na goli hakika Ahly walipewa mechi nzuri na waliulizwa maswali magumu pia.