Hii ni CROWN MEDIA, 92.1 CROWN FM & CROWN TV Follow us on Social Media Platforms Instagram: Crown FM - https://www.instagram.com/crownfmtz/ Crown TV - https://www.instagram.com/crowntvtz/ Twitter (X): CROWN MEDIA SWAHILI: https://twitter.com/CrownMediaTZ CROWN MEDIA ENGLISH: https://twitter.com/CrownMediaEN Facebook: CROWN MEDIA: https://www.facebook.com/profile.php?id=61556920898213&sk=followers TIKTOK: - https://www.tiktok.com/@crownmedialive?lang=en SUBSCRIBE & WATCH OUR SHOWS: https://www.youtube.com/channel/UCWHlCJN-WTamGWp4E6ZrhsA
#Simbasc #wachezajiwapyasimbasc #Ahmedally WACHEZAJI WAPYA WALIOSAJILIWA SIMBA MSIMU HUU 2026/2027 Waliosajiliwa 1. Kaletso Makgalwa Winga kutoka Shekukune 2.Serge Badjo kutoka Ivory Coast Mlinzi wa kati Sababu ni Rushine injury aliyopata fainal dhidi ya Azam CRDB imemfanya atachelewa kurejea uwanjani 3. Ibraheem Jabaar kiungo kutoka Stellenbosch alifanya kazi na Steve Berker 4. Nathaniel chilambo kutoka Azam FC ameshatambulishwa ndiye mrithi wa Kapombe Simba 5. Kelvin Nashon kutoka Singida BS ila alikuwa Kwa Mkopo Pamba Jiji 6.Bakari Msimu kutoka Coastal Union 7. Ismail Mgunda Mshambuliaji kutoka Mashujaa 8.Seleman Mwalimu imeshindikana kusajiliwa mazima kutoka wydad kutokana na wydad kutaka mpunga mrefu ila Simba wamekubaliwa kwenye Mkopo wa msimu mzima hivyo Seleman Mwalimu atasalia tena Simba Kwa Mkopo . Wanatazamwa kwenye kagame cup wakikidhi wanasajiliwa mazima 9. Ibrahim Doumbia Mshambuliaji raia Wa Mali, Ibrahim Doumbia amesaini mkataba wa mwaka mmoja ambao una kipengele cha kuongeza miaka miwili baadae katika klabu ya Simba Sc ya Tanzania. Doumbia alikuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mali Msimu ulopita akiwa na mabao 17. Simba hawataki kucheza kamali ya kumpa mkataba wa muda mrefu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, wakihofia akifeli na gharama za kuvunja mkataba. Doumbia msimu uliopita:- 🏆 Mfungaji bora wa Msimu 🏆 Mchezaji bora wa Msimu 🏆 Mchezo bora chipukizi wa Msimu. 🏆 Alikuwepo kwenye kikosi Bora cha msimu. DEAL OFF Ramadhan Chobwedo Winga kutoka TRA United amefeli vipimo vya afya Simba Dili lake limekufa rasmi Mpaka sasa Simba Sports Club imeachana na wachezaji wengi kuelekea msimu ujao. Je ni nani hakustahili kupewa Gudubaiii hapa utaniambia kwenye uwanja wa Comment hapo chini. 1. Chamou Karaboue. 2. Naby Camara. 3. Edwin Balua. 4.Joshua Mutale. 5. Awesu Awesu. 6. Omari Omari. 7. Moussa Camara. 8. Mzamiru Yassin 9. Ladack Chasambi 10. Jonathan Sowah 11. Mohamed Bajaber 12. Salehe Karabaka Mkopo Pamba Jiji 13. Valentino Mashaka Mkopo JKT Tanzania
Moshi. Mshambuliaji wa Simba SC na Taifa Stars, Selemani Mwalimu, ameshindwa kuzuia hisia zake na kuangua kilio wakati wa hafla ya ufunguzi wa Uwanja wa Mandela uliopo kata ya Pasua mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, iliyoandaliwa kuelekea kuanza kwa michuano ya Zuberi Cup 2026. Mwalimu amelia alipokuwa akisimulia maisha magumu aliyopitia kabla ya kufanikiwa katika soka, akisema uwanja huo una kumbukumbu nyingi za safari yake ya kutafuta mafanikio. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Mwalimu amesema akiwa pamoja na rafiki yake, Maulid, walikuwa wakifika uwanjani hapo usiku wa manane kufanya mazoezi licha ya kukosa vifaa muhimu, wakiamini siku moja ndoto zao zingetimia. "Huu uwanja una historia kubwa sana kwenye maisha yangu. Mimi na mshikaji wangu Maulid tuliteseka sana hapa. Kuna kipindi tulikuwa tunakuja kufanya mazoezi usiku wa manane tukiwa hatuna hata viatu, tukiamini ipo siku tutatoboa. Kurudi hapa leo nikiwa hivi, siamini macho yangu. Namshukuru Mungu sana," amesema Mwalimu huku akifuta machozi. Kauli yake iliyoambatana na kilio imegusa wengi waliohudhuria hafla hiyo, huku baadhi wakimshangilia na wengine wakionekana kuguswa na simulizi hiyo ya maisha yake.
Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania.