Kuelekea mechi ya Tarehe 13.6 ,kauli ya Julio ni hii. 🎙️JULIO, Mashujaa FC. 🗣️"Simba SC wao wana safu kali ya kushambulia kuliko Yanga SC, Yanga SC kwangu ni timu nyepesi Kabisa ila bado nawaheshimu, Dube ni mchezaji Opportunist sio Fighter, Pacome ana kokota vizuri, Mudathir ni mjanja mjanja, Ukiwawekea watu wa kuwakaba vizuri hawachezi, Goli 5 sio kwa Julio."- Jamhuri Kihwelo 'Julio' Head Coach Mashujaa FC. 🗣️"Yanga SC wanajua Kabisa wanaenda Kucheza na Kocha anaejiamini sana, sasa nilivyojiamini wakati ule na Simba SC ndivyo hivyo hivyo ninavyojiamini kwa Yanga SC."- Julio.
Tazama highlights jinsi Simba walivyobanwa mbavu na kulazimishwa suluhu na Dodoma jiji, mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania ukipigwa kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma.
WAPE TABASAMU: Team Kibwana kwa mara ya tatu imekula kichapo safari hii ikipigwa 6-2 na Team Job katika mchezo wa hisani wa #WapeTabasamu2024 uliopigwa Uwanja wa jamhuri. Morogoro. Magoli ya Team Job yametoka kwa Eng. Hersi Said (13'), Said Ndemla (234'), Prince Dube (27'), George Mpole (78'), Samson Mbangula (79') na Edwini , Balua 90'+4. Magoli yote mawili ya Team Kibwa yamefungwa na Saimon Msuva dakika ya 30 kwa free-kick na dakika ya 47 kwa penati. Haya hapa magoli yote manane.
Leo Juni 14 Ally Kamwe,Kibwana,Job, na kamati nzima ya Wape Tabasamu wamezungumza kuelekea Mchezo wa Wape Tabasamu 2024 ambao utapigwa Mkoani Morogoro ukikutanisha Timu Kibwana Dhidi ya Timu Dickson Job kwenye Uwanja wa Jamhuri
Stephane Aziz Ki amefunga magoli mawili na kufikisha magoli 17 katika mbio za ufungaji bora, Yanga ikiibugiza Dodoma Jiji mabao 4-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Ni mchezo wa #NBCPremierLeague uliofunguliwa na goli la Clement Mzize dakika ya 10 kabla ya Aziz kufunga mawili dakika ya 45+3 kwa penati na dakika ya 51, na kisha Maxi Nzengeli akafunga kazi kwa goli la nne dakika ya 78. Magoli yote manne haya hapa....
Goli pekee la Freddy Michael Koublan limeipa Simba pointi tatu muhimu, wakiichapa Dodoma Jiji 1-0 kwenye Dimba la Jamhuri, Dodoma. Hii ni #NBCPremierLeague