SIMBA SC 0-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (23/11/2018)
SIMBA SC 0-0 LIPULI FC; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (23/11/2018)

Ligi Kuu Soka Tanzania Bara imeendelea leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mabingwa watetezi Simba wamelazimishwa suluhu na Lipuli FC kutoka mkoani Iringa. Mchezo huo uliokuwa mkali na wenye ushindani, ulitawaliwa na kosakosa kila upande ambapo Simba walipoteza nafasi zaidi ya nne kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco, huku Lipuli walipoteza nafasi takriban tatu walizopata kutokana na makossa ya beki wa Simba Paul Bukaba. Makosa ya beki huyo yalimlazimu kocha wa Simba kufanya mabadiliko kwa kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na James Kotei dakika ya 38 ya mchezo. Kunako dakika za nyongeza, Meddie Kagere alikuwa ameshatikisa nyavu za Wanapaluhengo Lipuli FC lakini kwa mujibu wa mwamuzi wa pembeni, ilikuwa ni 'off-side' hali iliyoonekana kuzua malalamiko kwa upande wa Simba. Mara baada ya mchezo Nahodha wa Simba John Bocco amesema kilichowakosesha ushindi ni kukosa bahati, huku Nahodha wa Lipuli Ally Mtoni akisema kuna mbinu ambazo wao huzitumia kila wanapokutana na timu kubwa ili kupata pointi. Matokeo hayo ambayo ni mwendelezo wa rekodi ya Kocha wa Lipuli Selemani Matola kutofungwa na Simba yameiacha Simba ibaki katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 27 baada ya kucheza mechi 12.



MAGOLI: LIPULI FC 1-1 STAND UNITED (TPL - 05/10/2018)
MAGOLI: LIPULI FC 1-1 STAND UNITED (TPL - 05/10/2018)

Timu ya Lipuli FC ‘Wanapaluhengo’ wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Chama la wana Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa samora mjini Iringa. Wageni Stand United ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 48 kupitia kwa Sixtus Sabilo akitumia vyema uzembe wa mabeki wa Lipuli ambao walisahau kumkaba, lakini ‘super sub’ Issa Rashid aliyeingia kipindi cha pili aliisawazishia Lipuli FC bao dakika ya 79 akimalizia mpira wa kona kwa kichwa. Haya hapa magoli.



LIPULI FC 0-0 AZAM FC, (HIGHLIGHTS & INTERVIEWS) - 16/02/2018
LIPULI FC 0-0 AZAM FC, (HIGHLIGHTS & INTERVIEWS) - 16/02/2018

Timu ya Azam FC imeshindwa kutamba mbele ya Wanapaluhengo, Lipuli FC ya Iringa kwa kulazimishwa suluhu katika mchezo wa raundi ya 19 ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Wakicheza kwa kiwango kizuri uwanjani kwao Samora mkoani Iringa, Lipuli FC wameibana vilivyo Azam huku wakishindwa kutumia nafasi takriban tatu za wazi. Lipuli pia wamewazidi Azam umiliki wa mpira, wakimaliza mchezo wakiwa na umiliki wa asilimia 51 dhidi ya 49 za Azam.





Popular Tags

#Golden State Warriors  #Football Defensive Skills  #LeBron James  #Best Football Defending Skills  #Kevin Durant  #Counter Attack Goals Football  #Goalkeeper Saves  #Cleveland Cavaliers  #Paul Pogba  #Ronaldinho  

Popular Users

#DjokerNole  #PMOIndia  #kobebryant  #SteveNash  #NASA  #MichelleDBeadle  #MieshaTate  #RobGronkowski  #incarceratedbob  #serenawilliams  #espn  #DeionSanders  #THNRyanKennedy  #shakira