Content removal request!


TANZANIA BARA 1-0 ZANZIBAR | HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (CECAFA SENIOR CHALLENGE - 10/12/2019)

Kumbukumbu za kupoteza pambano la mwisho kwenye michuano ya CECAFA kwa Tanzania Bara mbele ya Zanzibar zimefutika wakati timu hizo mbili zilipokutana leo na Bara kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao pekee la Bara limewekwa kambani na mshambuliaji Ditram Nchimbi dakika ya 39 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Zanzibar kufuatia krosi ya Eliuter Mpepo. Kwa matokeo haya Stars ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza wanaweka kibindoni alama tatu ,wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Kenya wenye alama sita ,wakati Zanzibar wao wanasalia na alama yao moja iliyotokana na sare ya mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan. Kutokana na kundi hilo kufikia hatua ngumu kwa sasa makocha wa timu zote mbili wanafahamu umuhimu wa michezo hiyo ya kuhitimisha hatua ya makundi.