Content removal request!


STAND UNITED 1-1 KAGERA SUGAR; HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 14/12/2018)

Stand United imegawana pointi na Kagare Sugar kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Wenyeji Stand United ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Datus Peter baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Kagera Sugar. Kagera Sugar ambao walionekana kucheza vizuri zaidi hasa kipindi cha kwanza, walitulia na kufanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake Jerson Tegete, akimalizia pasi ya Ramadhan Kapera.